"Kupitia elimu mliyoipata tunategemea kuona mambo yanakuwa motomoto huku shambani,"
Hayo yamesemwa leo Aprili 29, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule alipofanya ziara ya kukagua mradi wa kilimo wa vijana ambao uko chini ya wizara ya kilimo unaokwenda kwa jina la bbt. Mradi huu unatekelezwa Chinangali wilaya ya Chamwino.
Amewataka vijana hao pamoja na kuwa na mikakati ya kulima mazao ya muda mrefu wawe pia na mkakati wa kulima mazao ya muda mfupi kama vile mbogamboga zitakazowasaidia kukidhi mahitaji madogomadogo ya kila siku.
"Kuanzia Dodoma kwenyewe kuna mahoteli mengi, kuna mahitaji mengi ya vyakula. Naamini hata leo mkiwa mnagawana watano waende kwenye mahoteli,mkatembee kwenye viwanda, hapa mnawaletea nyanya, mnajua ni kiasi gani na vitu vingine vya kawaida. Mambo mengineya wiki mbili, mwezi yanapaswa kuwepo kwa sababu mnatakiwa kuishi kila siku. Kwahiyo nendeni mkatafute masoko kuanzia yale madogo, ya kati na hata makubwa." Alisema Mkuu wa mkoa.
Vilevile alikumbushia suala la kupanda miti kuzunguka kwenye mashamba ili kuzuia upepo shambani na kutunza mazingira jambo ambalo ameona halijatekelezwa na kuwaelekeza wafanye hivyo.
"Nimesikitika ile juhudi tuliyoifanya imekuwa kama ya kulazimisha. Tulileta miti kupitia TFS lakini hatukuendelea na mwaka huu kulikuwa na mvua nzuri sana za juweza kumwagilia ile miti. Kwa hiyo nitoe shime wakati huu mnapoendelea kusubilia vitu vingine basi kwenye hizo 'block' waendelee kupanda miti, waimwagilie ili iendelee kuwa kinga upepo kama mnavyoona kule kwenye zabibu inafurahisha na inakuwa haraka lakini hata mashamba yanapendeza pamoja ni mashamba ya kilimo lakini yawepia kwa ajili ya utalii wa kilimo." Alisema mkuu wa mkoa.
Mkuu wq mkoa pia amewataka vijana kuilinda Nchi kwa kuwa wanaotakiwa kuilinda ni vijana wenye nguvu.
"Ninyi hamtailinda Tanzania kwa mtutu bali kwa uhakika wa chakula, mtailinda kwa uhakika wa uchumi kwa maana ninyi mmewekewa mazingira ya kujipatia uchumi lakini uchumi kwa ajili ya Taifa. Na kuilinda huko ni kwa kufanya bidii kwa uaminifu na uadilifu lkini kulinda huko ni kwa kusema mabo mazuri ya nchi yako." Alisema Mhe. Senyamule.
Aidha mkuu wa mkoa ametembelea eneo la shamba zima pamoja na eneo la kiwanda cha kukamua mchuzi wa zabibu ambacho ni sehemu ya mradi huo wa kilimo na ametoa maelekezo ambayo wataalam wanapaswa kuyafanya ili mradi uweze kutekelezwa kwa ufanisi
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.