Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 22 Januari, 2025 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari kijiji cha Igandu.
Mhe. Rosemary Senyamule aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mhe. Janeth Mayanja, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito Mganwa pamoja na Menejimenti kukagua mradi huo wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Igandu.
Akizungumza katika ziara hiyo RC Senyamule ameagiza kukamilishwa kwa haraka ujenzi wa Shule hiyo ifikapo tarehe 31 ya mwezi Januari ili kuwapunguzia umbali mrefu wa kutembea kwa wanafunzi kutoka katika kijiji cha Igandu ambao hutembea kilomita 9 kwenda katika shule ya sekondari Nghahelezi.
Sanjari na hilo, Mhe. Senyamule ametoa rai ujenzi wa shule hiyo kuendana na fursa za kiuchumi zinazopatikana katika eneo hilo kutokana na uwepo wa stesheni ya treni ya mwendokasi (SGR) ya Igandu karibu na shule hiyo, hivyo kuomba kutengwa kwa eneo kwa ajili ya fursa za uwekezaji.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amemshkuru RC Senyamule kwa kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Igandu pamoja na kumuhaidi Wilaya ya Chamwino kuongeza jitihada katika usimamizi wa miradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.