Na Brian Machange-Chamwino
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Deo Ndejembi amesema serikali kupitia wizara yake haita wavumilia Maafisa Utumishi wazembe na wanaojifanya miungu watu wanaowaonea watumishi katika utumishi wa Umma.
Naibu Waziri Ndejembi ameyasema hayo Aprili 15, 2021 alipofanya ziara ya kawaida ya kikazi Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma na kukutana na watumishi wa Halmashauri ya Chamwino kwa lengo lakufanya nao mazungumzo na kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo katika kutimiza majukumu yao ya kila siku maeneo yao ya kazi.
Wakizungumza katika ziara hiyo, watumishi wamemueleza Waziri Ndejembi kuwa matatizo mengi wanayokumbana nayo niyakiutumishi kama vile kukaa muda mrefu bila kupandishwa madaraja hali inayopelekea kushusha morali ya utendaji kazi kwani kuna watumishi ambao zaidi ya miaka saba hawajapandishwa madaraja na wengine wanamadai ya muda mrefu ambayo sio ya mishahara kama vile uhamisho na stahiki nyingine.
Kuhusiana na hoja za watumishi hao, Mhe. Waziri Ndejembi amewahakikishia kuwa serikali iko bega kwa bega na watumishi kwa kutambua mchango mkubwa wanaoutoa kwa Taifa,hivyo kwakutambua mchango wa watumishi serikali imejipanga kuwapandisha wadaraja wafanyakazi wote wapatao 90,000 kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022.
Mhe. Naibu waziri Ndejembi ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wote nchini kufanyakazi kwakujituma ilikuongeza tija katika maeneo yao yakazi na kuwataka kila mtumishi kuwa na mpango kazi unaomuongoza kila wiki nini atafanya akiingia ofisini, kwa kufanya hivyo itarahisisha kujifanyia tathmini binafsi na taasisi husika.
‘Sio mnachekelea kuona sisi serikali tunawapandishia madaraja ilihali nyie utendaji wenu wa kazi hauridhishi, Ofisi ya Rais-Utumishi haitomvumilia mtumishi yeyote ambaye ataleta uzembe kazini pamoja na Maafisa Utumishi atakaye kuwa akiwaonea watumishi wa umma’ Amesema Naibu waziri Ndejembi.
Nisisitize tubadilike, haya malalamiko yanayotolewa kwa Maafisa Utumishi kuwa hawapeleki kwa wakati changamoto za watumishi wao kwenye mamlaka husika, hawatumi majina ya watumishi wanaopaswa kupandishwa Madaraja, hii changamoto tumeiona nchi nzima nirudie tena hatutavumilia wale wote wanaojiona miungu watu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.