Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amekabidhi mifuko ya simenti na mabati kwa ajili utekelezaji wa miradi kwa jimbo la Chamwino leo, Machi 10, 2023. Makabidhiano yamefanyika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Akikabidhi vifaa hivyo Mhe. Waziri amewataka waheshimiwa Madiwani na wataalam wote waliokabidhiwa vifaa hivyo kuhakikisha vinafanya kazi ya miradi iliyokusudiwa na inakamilika kwa wakati.
" Kubwa ambalo nasisitiza ni usimamizi wa vitendea kazi hivi viweze kutumika kama malengo yanavyotaka na mkiacha usimamizi ni kumaliza miradi kwa wakati na hii si tu kwa waheshimiwa Madiwani bali hata watumishi kwa ujumla".
" Changamoto kubwa tuliyonayo Serikali za Mitaa ni miradi ya Serikali kutokamilika kwa wakati lakini si tu kukamilika kwa wakati baki hata usimamizi waje huwa duni na ndio unakuta miradi inachelewa. Na hizi fedha zinaletwa na Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan ili zije kuhudumia wananchi na si kutuhudumia sisi viongozi."
Jumla yamifuko 1950 ya simenti na mabati 130 yamegawiwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo 30.
Alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteuwa kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI na àliahidi kufanya kazi kwa bidii kama matarajio Ya Mhe. Rais
Naye Diwani wa Kata ya Buigiri ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Keneth Yindi alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kutokana na mtumizi yaliyowazi kwa fedha za Mfuko wa Jimbo kwani vifaa hivyo vimegawiwa mbele ya Waheshimiwa Madiwani wote kwa kadri ya mahitaji yao waliyoyawasilisha.
" Mhe. Naibu Waziri wa TAMISEMI kwa niaba ya Halmashauri nashukuru kwa matumizi yaliyowazi ya fedha za mfuko wa jimbo.umeona suala hili liwe la wazi umewaita Madiwani wote na kila Diwani amepata kulingana na mahitaji yake na hii inaonyesha sisi ni wamoja na angeomba iwe mfano kwa maeneo mengine katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi."
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.