Action Aid Yakabidhi vifaa vya Kujikinga na Virus Vya Corona, Chamwino
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bibi Vumilia Nyamoga amekabidhiwa vifaa kwa ajili ya kujikinga na Corona vilivyotolewa na Shirika la Action Aid . Makabidhiano hayo yamefanyika jana, Juni 15, 2020 Ofisini kwake Chamwino.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni mavazi maalum yanayotumiwa na wahudumu wa afya wanapokuwa wakiwahudumia wagonjwa wa corona (PPEs) pea 50, matenki ya maji 14 na mashine za kunawia mikono 14.
Aidha Shirika hilo limekabidhi pia cherehani mbili (2) za kudarizi kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali wadogo.
Vifaa hivi vinatarajiwa kugawiwa kwenye maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ambapo matenki makubwa matatu (3) yenye ujazo wa lita 1000 pamoja na mashine tatu za kunawia kwa kila eneo yatapelekwa shule za msingi za Msanga, Mahama na Mlowa barabarani.
Vilevile Hospitali ya Wilaya Mlowa Barabarani imepewa matenki makubwa ya lita 1000 mawili (2), na mengine mawili (2) yamegawiwa katika vituo vya Afya vya Mpwayungu na Haneti.
Matenki saba (7) yenye ujazo wa lita500 pamoja na mashine saba (7) za kunawia yamegawiwa kwenye shule za Sekondari za Msanga, Mlowa barabarani na Buigiri pamoja na Zahanati za Dabalo, Ilangali, Champumba na Itiso.
Mgao wa cherehani ulikwenda kwenye kikundi cha Nyota njema kilichopo Kata ya Chamwino na umoja kilichopo kijiji cha Mlodaa.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo walioutoa na kuelekeza kuwa vifaaa vitunzwe vizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.