Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amezindua matumizi ya kompyuta na printer, Agosti 17,2022 zilizonunuliwa kupitia kampeni ya NISHIKE MKONO KUINUA UBORA WA ELIMU CHAMWINO ambayo ilianzishwa na yeye mwenyewe.
Uzinduzi wa vifaa hivyo vya kompyuta umefanyika shule ya msingi buigiri ambapo mashine hizo zitagawiwa kwenye shule nne za msingi pamoja na ofisi ya Mratibu Elimu Kata kwa ajili ya kuchapa na kudurufu mitihani ambayo itasaidia katika kuwaandaa wanafunźi kufanya vizurk kwenye mitihani yao ya kitaifa na hivyo kuinua ubora wa elimu.
Akizungumza kwenye hafla hio amewapongeza na kuwashukuru wote waliochangia Kampeni hiyo ambapo kila kaya ilipaswa kuchangia kiasi cha shilingi elfu tano. Alisema jumla ya michango iliyopatikana ilikuwa ni shilingi milioni 107 na kata ya Buigiri iliweza kuchangia kiasi cha milioni 7.6
Aidha alieleza kuwa kupitia wadau waliweza,kukusanya kiasi cha shilingi milioni 28 ambazo ziligawanywa kwenye kata zilizofanya vizuri kwenye kukusanya michango ikiwemo kata ya buigiri.
Kata ya buigiri ilipatiwa shilingi milioni 4 ambazo zilipelekwa shule shikizi ya Mizengo pinda ambayo wananchi walijitolea hali na mali kujenga madarasa na Serikali kupita Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupeleka milioni 60 kwa ajili ua kujenga madarasa 3 na ofisi ya walimu na hivyo wakaona wawaongezee nguvu kwa ajili ya kukamilisha ili shule iweze kuanza.
Milioni 10 ilipelekwa sekondari ya Ikowa ili kukarabati madarasa 3 na ofisi ya walimu na baadae waliongeza shilingi milioni 3 kwa ajili ya matundu ya vyoo baada ya kuona hakuna matundu ya vyoo.
Vilevile ilitolewa shilingi laki 4 kuwasaidia wanfunzi shule ya Nhinhi waliofaulu vizuri ili waende kidato cha tano na sita ambao wazazi walishindwa kuwapeleka shule kutokana na haoi duni ya maisha.
Mkuu wa wilaya alimshukuru Mhe Rais kwa kuwapelekea kiasi cha shilinngi bilioni 2,9 fedha za UVIKO 19 ambazo zilijenga vyumba vya madarasa164. Walishirikiana na jamii kufanya kazi ambazo hazikuwa na ulazima wa kutumia fedha pekee na kufanikiwa kuokoa fedha iliyosaidia kujenga ofisi 75 za walimu na kupata madawati kwa vyumba vyote.
Aidha akieleza kuwa wamefanikiwa kupata usajili wa shule shikizi 4 kati ya tisa walizoziombea usajili. Nyingine hazikufanikiwa kutokana na kukosa matundu ya vyoo, hivyo wamekubaliana na Mkurugenzi wa Halmashauri waweke kwenye bajeti hii iliyaweze kujengwa na shule zisajiliwe kli mwakani zianze kusajili wanafunzi.
Sambamba na kuzindua vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya pia amezindua mfumo ambao utatumika katika kuandaa mitihani ya kuwapima wanafunzi pamoja nakuona mahudhurio yao
Pia bendera nyekundu anbayo itapeperushwa kwa wazazi ambao hawatawapeleka watoto shuleni na ofisi ya kijiji ambayo itakuwa na kaya nyingi ambazo hazikupeleka watoto shuleni. Baada ya hàpo sheria zitachukuliwa dhidi ya wazazi hao.
Wakiongea kwa nyakati tofauti katika hafla hiyo. Mhe. Diwani wa kata ya buigiri na Mtendaji wa kata wamesema ili kuboresha elimu wanafunzi hawataruhusiwa kutoka nje ya kata mpaka kwa kibali kutoka uongozi wa kata ili kuwabaini ambao hawataripoti shueleni kwa wakati ili waweze kutafutwa na kurudishwa shuleni.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.