Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Janeth Mayanja aliyehamia akitokea Wilaya ya Hanang amefanya kikao cha kutambuana na watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wilayani Chamwino.
Kikao kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Machi19, 2024 baada ya kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake Mhe. Gift Msuya ambaye amehamishiwa Wilaya ya Bahi.
Amesema lengo la kikao hicho nikutambuana pamoja na kusisitiza baadhi ya mambo ambayo anataka yapewe kipaumbele.
Mambo aliyoyasisitiza ni pamoja na uwajibikaji wa kila mmoja katika eneo lake la kazi ili kuleta tija na maendeleo yanayokusudiwa na Serikali kwa wananchi.
Vilevile amehimiza kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato ambapo ameitaka Kitengo cha Fedha na Idara ya Viwanda na biashara kuhakikisha wanasimamia vema suala hili na kuondoa mianyà ya upotevu wa mapato.
Aidha Mhe. Mayanja amesisitiza pia kuhusu suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo. Ameelekeza fedha za miradi zinàpoletwa zisimamiwe vizuri na kukamilika kwa muda uliopangwa ili kuepuka kuwepo kwa miradi iliyochini ya viwango na miradi viporo.
Ameelekeza isianzishwe miradi mipya kabla ya kukamilisha miradi viporo, amesema bajeti inapopangwa izingatie hayo.
Baada ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule maalum ya Wasichana ya Mkoa iliyopo kata ya Manchali.
Katika ziara yake hiyo ya Manchali Mkuu wa Wilaya aligawa Taulo za kike kwa wanafunzi waliopo shuleni hapo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.