Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Staki Senyamule amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa fedha za mradi wa Boost.
Ukaguzi huo umefanyika Mei 30, 2023 kwenye kata za Handali kijiji cha mjeloo ambapo inajengwa shule nzima yenye mikondo miwili na kata ya Makang'wa kijiji cha Makang'wa ambapo yanajengwa madarasa nane.
Akizungumza na wananchi Mkuu wa Mkoa amewahimiza kuchangia nguvu kazi kuunga juhudi za Serikali kama walivyokubaliana kwani kwa kufanya hivyo wataweza kupata fedha ya ziada ambayo inaweza kufanya kazi nyingine ya maendeleo kwenye shule zao.
"Nawasihi wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia maendeleo kwani hayana mwisho na wala hakuna mwisho wa kufanya kazi hivyo mjitume"
Akiwa Handal amepongeza kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa na amewahimiza mafundi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo kwani yanatakiwa kukamilika na kukabidhiwa kwake ifikapo Juni 20, 2023 na wizarani majengo yanapaswa kukabidhiwa Juni 30, 2023.
Aidha mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara ambapo amepokea na kujibu kero mbalimbali za wananchi
Vilevile Mkuu wa Mkoa amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwapelekea wananchi maendeleo na amewaomba wananchi kuendelea kuyatangaza mazuri hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.