Mwenge wa Uhuru ukiongozwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Eliakim Mzava leo umefika Wilayani Chamwino aambapo umetembelea, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba.
Miradi hiyo ni pamoja na.mradi wa kuhifadhi.mazingira kitalu cha miti ikowa uliopo kijiji cha Bwawani kata ya Manchali ambao umetembelewa wenye thamani ya Tsh. 86,957,600.
Mradi mwingine ni mradi wa jengo la OPD kituo cha Afya Msamalo uliopo kijiji cha Mgunga Kata ya Msamalo ambao umewekewa jiwe la msingi. Mradi umegharimu kiasi cha shilingi 167,427,1138.86
Mwenge wa Uhuru pia umetembelea shule ya msingi Buigiri Blind, shule yenye watoto wenye mahitaji maalum iliyopo kijiji cha Buigiri ambapo watoto wamepatiwa kadi za matibabu za bima ya Afya zenye thamani yashilingi 2,000,000/-
Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya lami ya Nelsoni Mandela yenye urfu wa kilomita 0.7 uliopo kijiji cha Chamwino wenye thamani ya shilingi milioni mia 649,461,064
Mradi mwingine ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Mwl. Nyerere iliyopp kijiji cha Chamwino ambayo imezinduliwa ambayo imejengwa kwa thamani ya shilingi milioni 545,675,280.
Aidha Mwenge wa Uhuru umetembelea mradi wa maji kijiji cha Igamba ambao umetekelezwa kwa thamani ya shilingi milioni 347,298,170/_-
Mwenge wa Uhuru vilevile umetembelea kikundi cha vijana cha maafisa usafirishaji ( bodaboda) kijiji cha Igamba ambao umegjarimu kiasi cha shilingi milioni 13,100,000./-.
Aidha jana wameweza kupatiwa elimu kuhusu fursa za kiuchumi kwenye kongamano maalum lililoandaliwa kwa ajili ya vijana.
Mwenge wa Uhuru 2024 unaongozwa na Kauli mbiu inayosema " Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".,
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.