Halimashauri ya wilaya ya Chamwino imefanya mkutano wake wa Baraza la Madiwani wa robo ya tatu 2023/2024 leo Aprili 30, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Akitoa salamu za Serikali Mhe. Janeth Mayanja mkuu wa Wilaya ya Chamwino amewasihi Wahe. Madiwani kushirikiana na menejimenti katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Serikali inatoa fedha nyingi za miradi, na miradi hiyo inatekelezwa kwenye maeneo yenu, niwaombe hata kama kuna kamati za usimamizi, hata kama kuna Taasisi zinasimamia miradi lakini kwa kuwa ninyi ndio mko kule ninyi msijali kama ni mradi wa barabara, kama ni mradi wa darasa, msijali kama ni mradi wa umeme. Kama mwakilishi wa wananchi unajukumu la kuweka msukumo ili mradi uweze kukamilika kwa wakati." Alisema Mkuu wa Wilaya.
"Pale mnapoona mambo hayaendi vizuri ofisi yangu iko wazi ili tuweze kutatua changamoto hizo kwa pamoja mapema. Inakuwa ni vibaya wakati mwinginewanakuja viongozi wa mamlaka zingine za juu wanafika wanakuta kuna mambo hayaendi vizuri ili adhima ya Serikali ya utoaji wa fedha iende sambamba na upatikanaji wa huduma kwa wananchi." Aoisema Mkuu wa Wilaya.
Ameomba pia Halmashauri kuendelea kujipanga kuibua vyanzo vipya vya mapato kutokana na Halmashauri kuwa na eneo kubwa na hivyo kuwa na gharama kubwa za uendeshaji kuliko kwenda kupeleka miradi ya maendeleo kwa wanachi, lakini vyanzo vilivyopo kuvikusanya vizuri.
Alishauri Halmashauri kuanzisha nfuko wa elimu ili wadau wa Halmashauri wlioko nje na ndani ya Halmashauri wanaweza kuchangia chochote kwenye mfuko wa elimu ili watoto wanaotoka katika mazingira magumu waweze kusaidiwa na mfuko huu. Japo kuanzisha jambo hili si jqmbo la muda mfupi lakini ni vema wakalichukua na kulifanyia kazi.
Amezungumzia pia suala la utoro na kushauri kuwa na sheria ndogo ya kushughulika na suala la utoro.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Chamwino ndg. Malima ameomba walichukulie uzito suala la uvamizi wa simba na tembo kwenye Tarafa ya Mpwayungu ili wawe na amani kwenye makazo yao. Vilevile naye pia alisisitiza kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato.
Katika mkutano huo pia Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Ndg. Kasper Mamuya amewaomba wajumbe wote kuzibeba kero za wananchi na kuziona ni za kwetu na kuzishughulikia kwani ndio agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani. Na mkoa umejiwekea Kauli mbiu ya "kero yako wajibu wangu".
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.