Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja akiongozana na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ameshiriki zoezi la kuteketeza gunia tisa na shamba la ekari mbili za bangi lililopo katika mmoja ya mlima katika Kata ya Membe, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 15 Juni, 2025 kwa kufyeka na kuchoma moto shamba hilo la bangi huku Mhe. Janeth Mayanja akiwahasa Wananchi wa Membe na Chamwino kwa ujumla kuhakikisha wanaachana na kilimo haramu na kujikita katika kilimo halali ili kujipatia kipato halali na chakula.
Aidha, Mhe. Mayanja amesema zoezi hilo litaendeshwa katika vijiji vyote Wilaya ya Chamwino ili kuhakikisha wanatokomeza zao hilo haramu na kuwachukulia hatua wale wote watakaokutwa na hatia ya kulima zao hilo la bangi.
Kwa upande wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wamewahasa Wananchi kuachana na kilimo cha bangi na kutoa taarifa katika Mamlaka husika pale wanapoona zao hilo linalimwa katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.