Na Brian Machange - Chamwino
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo tarehe 11 Disemba 2020, limefanya Mkutano wake wa kwanza katika ukumbi wa Ofisi za Kijiji cha Chamwino Ikulu na kumchagua Diwani wa kata ya Mvumi Makulu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Edson Mdonondo kwa kura 51 kati ya 51 zilizopigwa hivyo kumfanya kushinda na kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino.
Aidha Baraza hili limemchagua Diwani wa kata ya Buigiri Mhe. Kenneth Yindi kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kura 51 kati 51 zilizopigwa.
Akiongea baada ya Ushindi huo, Mhe. Mdonondo alitoa shukrani za dhati kwa Chama chake na Waheshimiwa Madiwani wote waliomuamini na kumpigia kura na kuahidi kushirikiana nao katika kuwatumikia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Vumilia Nyamoga amesema kuwa Uchaguzi umeisha na kazi inayofuata ni ya Madiwani kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria, kanuni na maelekezo. Aidha amewataka kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Kwanza 2021 wanaripoti shuleni mara shule zitakapofunguliwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino Bw. Athuman Masasi amempongeza Mwenyekiti na Makamu wake kwa ushindi wa kishindo pamoja na waheshimiwa Madiwani na kuwahakikishia kutoa ushirikiano kwa yale yote watakayokuwa wanajadiliana kwenye vikao wanayatekeleza kwa wakati na kwa ufanisi wa hali ya juu.
Madiwani wateule wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakila kiapo leo tarahe 11 Disemba 2020.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Chamwino wakiwa katika mavazi yao maalumu tayari kwa kuanza kikao mara baadaya kuapishwa leo tarehe 11 Disemba 2020 katika ukumbi wa Ofisi za kijiji cha Chamwino Ikulu.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.