Na Brian Machange - Chamwino
Katika kutekeleza agizo la Serikali lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) tarehe 08.12.2020 kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa na Madawati (Viti na Meza) kwa shule za Sekondari zinatatuliwa kama sehemu ya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wote wa kidato cha Kwanza kwa mwaka 2021, Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mhe. Deo Ndejembi kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya hiyo ametoa zaidi ya shiling Milioni 2 katika tarafa za Itiso na Chilonwa ilikusaidia ukamilishaji wa vyumba vya madarasa ikiaa zimebaki wiki chache kabla ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema Januari mwakani.
Mhe. Ndejembi amekabidhi sh.600,000/= kwa shule ya Buigiri, sh. 500,000/= kwa shule ya Manchali, sh. 600,000/= kwa shule ya Chamwino, madawati 10 yenye thamani ya sh. 350,000/= kwa shule ya Msanga na mifuko 20 ya saruji yenye thamani ya sh. 340,000/= kwa shule ya Chilonwa.
Wakati huohuo Mhe. Ndejembi ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa shule za Itiso na Haneti kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa mara baada ya kupokea taarifa ya upungufu uliopo kwa shule husika, hata hivyo amezitaka shule za Sekondari Dabalo, Segala na Membe kukamilisha tathmini za kitaalamu kulingana na uhitaji wa shule hizo na kumpelekea taarifa hizo iliaweze kuchangia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino Mhe. Keneth Yindi amemuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Chamwino kwa kuahidi kuchangia zaidi ya laki 2 pamoja na kutoa mifuko 10 ya saruji na tripu 2 za mchanga ilikukamilisha ukarabati wa vyumba vya madarasa katika tarafa za Chilonwa na Itiso.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndejembi amewakilishwa na msaidizi wake Ndg. Muhsin Mulokozi aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Keneth Yindi, Mkuu wa Idara ya Sekondari Bi. Rehema Nahale, Afisa toka idara ya Sekondari Bi. Nyemo Masimba pamoja na Afisa Tarafa ya Itiso Ndg. Remedius Emanuel.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.