Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amefanya uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura Jimbo la Chamwino Septemba 21, 2024 ambao umefanyika kwenye kiwanja cha michezo kikichopo kijiji cha Chamwino.
Akizungumza katika uzinduzi huo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa wanaojiandikisha kwa mara ya kwanza ambao wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na kwa ambao watakuwa wametimiza miaka 18 mwakani 2025 kipindi cha uchaguzi na pia kwa wale watakaokuwa wanaboresha taarifa zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuhama maeneo waliyokuwa wakiishi zamani.
Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wamejiwekea mazingira ya kuweza kuchagua viongozi wao kama vile Madiwani, Wabunge Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani 2025.
Amewaomba wananchi waitumie nafasi hiyo vizuri ili mwakani wasisimuliwe bali wao wenyewe waweze kushiriki kupiga kura.
Vilevile mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba 2024 ambapo uandikishaji wake unatarajia kuanza kufanyika kuanzia tarehe 11hadi 20 Oktoba 2024.
"Kila aliyefika hapa akawe balozi kwa kufikisha ujumbe huu kwa watu waliknyuma yake ili bao waweze kushiriki kwenye zoezi hili la kujiandikisha kwenye nazoezi yote haya hawili." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Uzinduzi ulitanguliwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Veterani Fc na Buigiri Fc ambapo Veterani Fc waliibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri. Zilitolewa zawdi za mpira mmoja mmoja kwa kila timu na pesa taslim, Vilevile pesa taslim kwa marefa na kamisaa wa mchezo huo.
Aidha burudani nbalimbali za ngoma ziliupamba uzinduzi huo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya pia alizindua zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura kwa jimbo la Mvumi napema asubuhi ya Septemba 21, 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.