Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amewapongeza waheshimiwa Madiwani kwa kazi kubwa wanayoifanyakwenye maeneo yao,. Pongezi hizo amezitoa alipokuwa akitoa salamu za Serikali kwenye mkutano wa mwaka wa baraza la Madiwani Agosti 28, 2024 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Akitoa salamu hizo Mkuu wa Wilaya amewakumbusha Wahe. Madiwani kusimamia miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao itekelezwe kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa.
"Niwaombe wah. Madiwani ile miradi imepangwa kwa muda maalum wa utekelezaji, kwa kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwenye maeneo yetu, nyie muwe watu wa kwanza kufuatilia kuhakikisha miradi hiyo iweze kutekelezwa kwa wakati uliopangwa." Alisema mkuu wa Wilaya.
Aidha ameshauri Mkurugenzi mtendaji kufanya tathimini ya ndani ya Wilaya kwenye miradi yote kujuwa iwapo tunamaliza miradi kwa wakati, kata zilizochelewesha na kata zilizomaliza kwa wakati na watendaje wake wapate pongezi.
Ameelekeza changamoto zinapojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi ni vizuri kuhabarishana ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa tija iliyokusudiwa, na hiyo ni kwa miradi yote hata ile inayotekelezwa na taasisi nyingine pamoja na wakandarasi.
Aidha Mhe. Mayanja ameongelea suala la kupokea wageni kwenye wilaya ambapo ameelekeza wageni kutoa taarifa kwa watendaji wa vitongoji na mwenyekiti wa kitongoji kuzipeleka taarifa hizo kwa mwenyekiti wa kijiji ili wilaya iendelee kuwa salama.
"Kwa kufanya hivyo pale kutakapokuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani na vitu vinavyoendana na hivyo itakuwa rahisi kuchukuwa hatua." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa wilaya alizungumzia wimbi la watoto kuibiwa na kuwaomba wahe. Madiwani kuwatoa hofu wananchi na kuwaelekeza kutochukua sheria mkononi badala yake wawatumie viongozi waliopo kwenye maeneo yao kama wenyeziti wa vitongoji, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji, polisi kata na viongozi wengine.
"Inawezekana mtu amekuja kijijini anashughuli zake nyingine, kununua mazao,mifugo, hata mtu hqmjamuuliza mnasema huyu amekuja kuiba mtoto. Watu wakijichukulia sheria mkononi maana yake na wao watachukuliwa hatua, kwa hiyo wananchi wanaweza kujiingiza kwenye mgogoro usio wa lazima." Alisema Mhe. Mayanja.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.