Kufuatia maelekezo ya Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania katika uzinduzi wa mfumo wa uhasibu ngazi ya vituo (Facility Financial and Accounting System) na Planrep ya web-base kuwa Halmashauri zote nchini zitowe mafunzo kwa watumishi ngazi ya vituo na kuanza kutumia mfumo wa FFARS.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kupitia ufadhili wa Shirika la Health Promotion and System Strenghthening (HPSS) ilifanya mafunzo kwa watumishi wa Afya ngazi ya vituo 63 kwa kila kituo kuwakilishwa na mtumishi mmoja kuanzia tarehe 24 – 27 Oktoba, 2017 kwa kuwa na makundi mawili yaliyokuja kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilihudhuriwa na watumishi 29 tarehe 24-25 Oktoba na awamu ya pili 32 kuanzia 25- 27 Oktoba ambao walipatiwa mafunzo hayo ya FFARS kwa siku mbili kila kundi.
Mafunzo yaliendeshwa na wawezeshaji 5 kutoka ngazi ya Halmashauri na mwakilishi mmoja wa Shirika la HPSS. Watumishi walikuja na vifaa vyao pamoja na vitabu vyao vya kuingizia taarifa za fedha na kila mshiriki aliweza kuingia kwenye mfumo na kuanza kufanya mazoezi ya kuingiza taarifa kwa kuwa Halmashauri iliwezesha uwepo wa mtandao (wireless internet) katika ukumbi kuwezesha zoezi . Watumishi wote walikuwa kwenye mafunzo walifurahia mfumo pamoja na kuusifu namna unavyoweza kuwasaidia katika utekelezaji wa mipango ya vituo vyote.
Baada ya kufanya mazoezi, washiriki waliingia kwenye mfumo wa ‘live’ kwa password za na kasha kuanza kufanya kazi ya kuingiza Mpango wa kituo wa mwaka 2017/18 na kasha taarifa za kifedha za kuanzia 1 Julai, 2017.
Wakati wa Mafunzo, washiriki walipata kutembelewa na Meneja mradi wa Mkoa wa shirika la HPSS Bw. Kenneth Gondwe pamoja na mtaalam wa IT Bw Ishengoma kwa kuwapa maelekezo ya jinsi ya kutuma madai ya CHF.
Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alishukuru shirika la HPSS kwa ufadhili katika mafunzo ya FFARS na ushirikiano wao katika maendeleo ya Halmashauri ya Chamwino.
Mafunzo yalifungwa tarehe 27 Oktoba kwa watumishi kuhimizwa kwenda kukamilisha uingizaji wa taarifa za fedha kila siku kwatika mfumo na kuutumia ipasavyo na kuwaelekeza wenzao waliopo katika vituo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.