Wawakilishi wa vikundi vya wanawake kutoka kwenye kata 10 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya kuongeza thamani kwenye bidhaa za kilimo kama vile utengenezaji wa batiki, sabuni na mafuta kupitia mradi wa UN womeni unaosimamiwa na chemba ya biashara Tanzania (TWCC) wameaswa kuipeleka elimu hiyo kwa wengine waliobaki kwenye maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo kutoka mkoa wa Dodoma Bibi Honoratha Rwegasira Septemba 30, 2023 alipokuwa akifunga mafunzo kwa wanawake hao yaliyofanyika kuanzia tarehe 27 Setemba 2023 kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chamwino.
"Nachukuwa fursa hii kuwapongeza TWCC kwa hichi walichokifanya kwa kuchukua kata 10 baadhi ya watu kuja kushiriki kwenyemafonzo ni chachu, hivyo sisi kamawanajamii bado tunanafasi kubwa ya kwenda kuonesha kule tulikotoka." Alisema bibi Honoratha.
Aidha ameongeza kwa kufanya kazi waliyoyafundishwa wataweza kuongeza kipato kitakachosaidia kuondoa matatizo mengine kwenye familia.
Amewataka kina mama hao kutimiza majukumu yao katika familia kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea hata masuala ya ukatili waliyofundishwa kuondoka kwenye familia.
"Ukatilia wa kijinsia unatokea pale ambapo mwanamke hachukui nafasi yake, na amani isipokuwepo watoto ndio watakaoangamia na ndio tunu yetu." Alisema Bibi Honoratha.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.