Wizara ya mifugo imepanga maeneo sita ya kuyafanyia maboresho. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na uvuvi Ndugu Tickson Nzunda alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo rejea kwa maafisa ugani Nchini.
Mafunzo hayo yameanza kufanyika Novemba 14, 2022 Wilayani Chamwino na yatafanyika kwa siku mbili.
Maeneo yaliyopangwa ni pamoja na afya ya mifugo ambapo jukumu walilonalo ni kuhakikisha mifugo inakuwa na afya bora. Pia alieleza kuwa jambo la kuchanja mifugo na kuogesha mifugo ni lazima.
"Jukumu letu kuhakikisha mifugo inakuwana afya bora Kitaifa na Kimataifa." Alisema Katibu Mkuu.
Aidha alieleza kuwa Wizara imegawa dawa ya ruzuku, na mikoa yote imepata. Kwa kufanya hivyo wataweza kudhibiti magonjwa. Alisisitiza sheria, kanuni na taratibu za ufugaji bora ni lazima zizingatiwe.
Kuhusu kuimarisha huduma za ugani za mifugo alisema hilo ni jambo la lazima na ni lazima kuwe na mfumo wa utendaji wa wenye matokeo.
Jambo jingine lililopangwa ni kuimarisha suala la masoko kwa kuimarisha minada. Kuhakikisha mapato ya Halmashauri na Serikali yanapatikana.Aliongeza kuwa wafugaji ni lazima wachangie kwenye sekta ya mifugo.
Kwenye suala la malisho Katibu Mkuu alieleza kuwa ni lazima wafugaji waone juwa wanawajibu wa kupanda malisho. Serikali itaanzisha mashamba darasa ya malisho na kuwapa elimu wafugaji.
Jambo jingine ni kuimarisha ushirikishwaji wa huduma za ugani kwa sekta binafi na wafugaji wenyewe.
Vilevile wataimarisha mashamba ya Serikali ili yawe na mifugo bora na kuyafanya yawemya kibiashara. "Tujengeane uwezo ili kufuga kibiashara." Alisema Katibu Mkuu.
Kuimarisha ranchi za Kitaifa ili kudhibiti ufugaji holela. Wafugaji washirikiane na Halmashauri ili kupata maeneo ya kufugia kwa lengo la kufuga kibiashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.