Balozi wa Pamba nchini, Mhe. Agrey Mwanri, amewataka maafisa ugani kuwa elimisha wananchi kuhusu kilimo cha pamba katika wilaya ya Chamwino ili waweze kufuata taratibu na maelekezo yaliyotolewa kuhusu kilimo hicho.
Akizungumza katika mkutano na maafisa ugani wa Wilaya ya Chamwino leo, 12 Septemba 2022, amesema kilimo cha pamba ni cha mkakati kitakacho leta maendeleo kwa wakulima na serikali kwa ujumla.
Amesema wameongeza jitihada zilizokuwa zinaendelea kuhusu kilimo cha pamba ili kuweza kupata mbegu na mafanikio yaliyo mazuri katika wilaya hii.
“Sisi tumeongeza jitihada zilizo fanywa na wakulima wadogowadogo ili tuweze kuendeleza na kuboresha kilimo cha pamba ilikupata mafanikio mzuri zaidi."
“Mkulima mdogomdogo anapaswa kushikwa mkono na kupewa hamasa zaidi, na kuwaelimisha wanananchi kuhusu huu mpango wa kwenda kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba unafanikiwa kwa kiasi kibwa zaidi,” amesema.
Mwanri amesema ziara waliyoifanya katika mkoa wa Dodoma na hasa katika wilaya hiyo ilitoa mafunzo ya njia bora ya kulima pamba ili mkulima aweze kupata manufaa kupitia zao hilo.
Aidha Mwanri ameushukuru uongozi wa Halmashauri kwa ushirikiano uliotolewa na muitikio mkubwa wa wananchi walio jitokeza kushiri mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na balozi huyo.
“Ziara yetu tuliyo ifanya katika mkoa huu wa Dodoma na katika wilaya hii ya Chamwino haikufanya kazi ya kulima pamba bali ilitoa mafunzo ya namna nzuri ya kulima zao la pamba ili kuweza kupata mafanikio kupitia kilimo hiki.
“Pia tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mkoa, Wilaya, na Halmashauri kwa kutoa ushirikiano na muitikio mkubwa kutoka kwa Wananchi katika kushiriki mafunzo haya,”amesema.
Hata hivyo alisema wakulima wanapaswa kufuata hatua na miongozo ya kilimo cha zao hilo, kwani ardhi na hali ya hewa ya chamwino inaruhusu kilimo cha pamba.
Katika kikao hicho pia Mwanri amegawa vifaa mbalimbali vya kilimo kwa maafisa ugani kwa niaba ya Waziri wa Klimo Mhe. Hussen Bashe. Vifaa vilivyogawiwa ni pamoja na bomba za kupulizia dawa, gumboots na makoti ya mvua ( rain coats).
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.