Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua mradi wa ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita million 2.5 lililopo katika kata ya Buigiri wilaya ya chamwino.
Akizungumza katika uzinduzi huo alisema tarehe 26, Aprili kila mwaka wananchi husherekea maadhimisho hayo ambapo kwa mwaka huu yatafanyika kwa kila mkoa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kupitia kwa Waziri mkuu Mhe Kasimu Majaliwa.
“Kila mwaka tumekuwa tukisheherekea siku hizi na mwaka huu tulipokea maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Wazitri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa, akitoa maelekezo ya namna ambavyo nchi yetu itaadhimisha maadhimisho ya miaka 59 ya muungano”,
“Na maelekezo hayo yalitutaka tusherehekee kwa ngazi za mikoa na wilaya lakini maelekezo mengine yalitutaka tuendelee kuadhimisha kwa namna mbalimbali za kushirikisha wananchi, kufungua miradi, kuwa na makongamano na huduma mbalimbali za kuwaeleza watanzania wajuwe nini Muungano, faida zake ni nini na wapi tunaelekea katika Muungano wa nchi hizi mbili kwa hiyo leo tupo hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho haya”, alisema Mhe Rosemary Senyemule.
Hata hivyo alisema wanachi wanapaswa kutunza, kuilinda na kuonyesha utashi kwenye utunzaji na utumiaji wa maji hayo kwa umakini na kuhakikisha miundo mbinu hiyo hayailiwi wala haichezewi.
Aidha ametoa wito kwa wanachi kulipa bili za maji ili kuendelea kuboresha na kuendeleza miundo mbinu ya upatikanaji wa maji na kupunguza kero zinazo patikana katika jamii.
“Nitoe wito kwa wananchi mnaoneda kutumia maji haya wengine wakisikia upatikanaji ni zaidi ya asilimia 100 wanasema sasa hata nikiacha bomba wazi hayatoisha, hapana maji ni bidhaa adimu maji yanatakiwa yaheshimiwe yatumike kwa umakini mkubwa”,
“Lakini jingine mlipe bili za maji lazima unapotumia maji kuhakikisha unalipia gharama ambazo zinatakiwa kuzirejesha ili uendeshaji wa miradi hizi ziwe endelevu”, alisema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.