Kituo cha Afya Dabalo kimeanza kutoa huduma ya upasuaji Oktoba 25, 2023 ambapo mama mjamzito alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kujifungua.
Taarifa hiyo ya kuanza kwa huduma za upasuaji kituo cha Afya Dabalo imethibitishwa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Chamwino Dr. Eusebius Kessy.
Mganga Mkuu ameeleza kuwa Mtoto wa kike mwenye uzito wa 3kgs alizaliwa, na wote mama na mtoto wanaendelea vizuri.
Vilevile ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na shirika la UNFPA kwa kuwekeza kwenye miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba.
"Tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNFPA kwa kuwekeza kwenye miundombinu na manunuzi ya vifaa tiba ikiwemo gari la wagonjwa." Alisema Dr. Kessy
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.