Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus H. Mashimba amekabidhi mashine ya kukatia na kuchomelea vyuma Novemba 14, 2022 kwa vijana wa kikundi cha WASAKA TONGE Kata ya Buigiri ambayo imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo amewataka vijana hao kupitia mashine hiyo inabidi wazalishe zaidi ya wanavyozalisha sasa. Aliwapongeza kwa kupata mashine hiyo na kuwa mfano bora kwa Wilaya yachamwino. Kufanya kazi kwa ushirikiano kama kikundi kinawapa matumàini Serikali.
kuhusu changamoto ya bei waliyoitoa alieleza kuwa hilo siyo tatizo kwani uanisababisha wewe mwenyewe kutokana na bidhaa unayoizalisha hivyo aliwashauri kuzalisha bidhaa bora na kuongeza gharama kwa jinsi bidhaa alizozalisha. Hivyo ongezeko la bei litumike kama fursa.
Alielekeza Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya kuhakikisha anasimamia vijana hao kupata tenda kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri.
"Afisa maendeleo simamieni vijana hawa wapeni tenda kwenye miradi ya Halmashauri ili waweze kujiimarisha zaidi na ninyi mfanye kazi usiku na mchana ili muweze kukamilisha hayo mahitaji." Alisema Dkt. Mashimba.
Naye Diwani wa kata ya Buigiri Mhe. Keneth Yindi amewaeleza vijana kuwa wanayobahati kupata mashine hiyo kwani ni Halmashauri chache sana zilizopewa mashine hizo na wao wakiwemo. Ameeleza kuwa ni Halmashauri 52 tu kwa nchi nzima na kwa mkoa wa Dodoma ni Halmashauri 3 tu ndizo źimeweza kupata mashine.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.