Wajumbe wa kamati ya kudhibiti UKIMWI wilaya ya Chamwino wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Keneth Yindi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wametembelea vituo vya tiba na mafunzo kwa wanaoishi na virus vya UKIMWI.
Shughuli hiyo imefanyika jumamosi Septemba 3, 2022 kwenye Kituo cha Afya Chamwino, Hospitali ya Mvumi Mission na Kituo cha Afya cha Mlowa Barabarani.
Wajumbe wameweza kuchangia na kutoa kadi za bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa ( CHF) kwa watoto wanaoishi na Vvu wapatao 230 kwa maeneo yote waliyoyatembelea.
Kituo cha Afya chamwino zimetolewa kadi kwa watoto 54, hospitali ya Mvumi Mission zimetolewa kadi kwa watoto 91 na kituo cha Afya cha Mlowa barabarani zimetolewa kadi kwa watoto 85.
Aidha watoto wamepewa mahusia mbalimbali ikiwemo suala la kusoma kwa bidii maana elimu ndio kitu cha pekee ambacho kinaweza kuweka usawa kwa wote katika jamii kati ya maskini na matajiri.
Akiongea na watoto hao Mchungaji Emmanuel Madeje ambaye pia ni mjumbe wa kamati alisema kilichowasukuma wao kama kamati kufanya jambo hilo ni upendo walionao kwa watoto hao. Akinukuu mistari ya Biblia alisema, " Mshike sana elimu, usimuache aende zake maana huyo ndiyo uzima wako."
" Silaha pekee itakayowasaidia katika maisha yao ni elimu. Elimu ndiyo itakayowapa heshima, hivyo ninyi mliopata fursa ya kuwa shuleni someni kwa bidii.^ Alisema Mchungaji.
Naye Mwenyekiti aliahidi kutoa zawadi ya vifaa vya shule kwa watoto watakaoshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi kwa wanafunzi hao. Pia alisisitiza watoto kuweka bidii kwenye elimu, kjjituma na kujiamini na hapo ndipo watakapopata heshima kwenye jamii
Aliwataka pia kuzingatia masharti yote wanayoelekezwa na madaktari wao likiwemo suala la kufuatilia masuala ya unywaji wa dawa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.