Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi Chamwino Yapewa Maelekezo ya Kudhibiti Corona
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bibi Vumilia Nyamoga ametoa maelekezo kwa Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi Wilaya ya Chamwino kuhusu kudhibiti na kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ( COVID - 19).
Maelekezo haya aliyatoa jana Machi 18, 2020 alipofanya kikao na Kamati hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino.
Maelekezo yaliyotolewa ni kuwa Viongozi wote katika ngazi ya Wilaya , Tarafa, Kata ,Kijiji na Vitongoji Wahakikishe wanatoa Elimu kuhusiana na Ugonjwa huu kwa Wananchi, pamoja na kusimamia maelekezo yote yanayotolewa na Serikali kuhusiana na Ugonjwa huu.
Vile vile amewaelekeza Viongozi wa Taasisi zikiwemo, Shule na Vituo vya kutolea huduma za Afya , Viongozi wa Dini wahakikishe pia wanatoa Elimu kwa Watu wanaowahudumia na kusimama maelekezo yote yanayotolewa na Serikali kuhusiana na Ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na kuhimiza suala la kunawa Mikono kwa kutumia maji safi tiririka na sabuni. Pia amesema kila mmoja kwa Imani yake amuombe Mungu ili Ugonjwa huu usifikie hatua ya kuondoa uhai wa ndugu zetu.
“ Kila Taasisi iweke maji safi tiririka na sabuni kwa ajili ya kunawa Mikono na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi watashirikiana kuahakikisha kila Taasisi inatekeleza Maagizo haya yote. “
Aidha ameelekeza kuwa Wananchi waepuke Mikusanyiko ambayo siyo ya lazima ili kujikinga na maambukizi.
Mkuu wa Wilaya ameelekeza pia wamiliki wa vyombo vya Usafiri kama daladala wanunue dawa za kutakasa mikono kuhakikisha wanawapaka abiria kabla ya kuingia kwenye vyombo vyao vya usafiri na wakati wa kushuka pia na hivyo hivyo ifanyike kwa wamiliki wa Nyumba za kulala wageni kwa wageni wanaolala kwenye nyumba zao.
Amewataka wamiliki wa Nyumba za kulala wageni wafuatilie na kutoa taarifa iwapo atatokea Mgonjwa mwenye ugonjwa wa Corona (COVID - 19) .Aliongeza kuwa kuna umuhimu wa kufanya uhakiki wa wageni wote wanaoingia katika nyumba zao za kulala wageni na kuendelea kuwahimiza kujikinga kwa wale ambao wako salama.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa Watendaji wa Kata,Vijiji na Maafisa Tarafa kusimamia maelekezo yote yaliyotolea na kutoa taarifa katika ngazi ya Wilaya kila Wiki na muda wowote zitakapohitajika na aliomba kila mmoja kuona wajibu wa kutoa taarifa pale inapohitajika.
Mwisho aliomba wadau watakaoguswa wasaidie kutoa mahitaji yanayohitajika katika kuhudumia wagonjwa wa Ugonjwa huu iwapo watagundulika.
Aliwashukuru Kampuni ya “YAPI MARKEZ” kwa kutoa mabango yanayoelimisha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.