Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh.Janeth Mayanja akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito P. Mganwa na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ameongoza zoezi la usafi kata ya Mvumi Misheni.
Maadhimisho hayo ya siku ya usafi duniani yanayoadhimishwa tarehe 20 Septemba ya kila mwaka yamefanyika leo Septemba 21 katika Wilaya ya Chamwino kwa kushirikisha pia wananchi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi katika maeneo tofauti katika kata ya Mvumi Misheni.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mh. Mayanja amewataka viongozi wa kijiji na kata kuweka utaratibu mzuri kuwakumbusha wananchi kushiriki usafi na kuwahasa wananchi kufanya usafi maeneo yao ya biashara na makazi yao.
Mh. Mayanja amewahimiza pia wakazi wa Mvumi Mission kuhakikisha wanajenga vyoo na kuwataka viongozi wa kata na kijiji kufanya ukaguzi wa nyumba zote kuwatambua wananchi wasio na vyoo ili kuweza kusaidiwa kisheria kujenga vyoo na kuondoa kero ya wananchi kujisaidia sehemu zisizo sahihi.
Aidha, zoezi hilo la usafi liliambatana na uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Wilaya ya Chamwino litakaloanza tarehe 25 Septemba hadi tarehe 01 Oktoba mwaka 2024. Mh. Janeth Mayanja amewaasa wananchi hao kujitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari la kupiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi wao.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.