Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Dkt. Eusebius Kessy ametoa wito kwa watumishi wa sekta ya Afya wilayani humo kuwaeleza wananchi juu ya faida watakazozipata wanapojiunga na CHF iliyoboreshwa.
Wito huo ameutoa leo tarehe 12 Septemba, 2019 kwenye kikao na Waganga Wafawidhi wa Zahanati na Vituo vya Afya vya Wilaya ya Chamwino kwenye ukumbi wa kijiji cha Chamwino Ikulu. Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
"Ukiachilia mbali CHF kuwa mfuko wenye gharama nafuu zaidi nchini, CHF hurudisha kiasi cha fedha kwenye Zahanati na Vituo vya Afya kulingana na idadi ya wananchi waliojiandikisha katika eneo husika. Fedha hizo zinasaidia ununuzi wa dawa na vifaa tiba. Twendeni tuwaeleze wananchi wajiunge" alisema.
Aidha Dkt. Kessy amewataka wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya Wilaya ya Chamwino kusimamia weledi wa taaluma yao na amekemea vikali tabia zilizopo kwa baadhi ya watumishi wachache wasiokuwa waadilifu, wanaotoa lugha chafu kwa wagonjwa na uzembe katika maeneo yao ya kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.