Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino Bi.Neema Nyarege amewataka Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuwaandaa kikamilifu watahiniwa ili waweze kupata ufaulu wenye tija wa daraja A mpaka C na kuondoa ufaulu wa alama D na E kwa ngazi ya shule za msingi.
Bi.Nyarege ametoa tamko hilo wakati akizungumza na Viongozi wa Sekta ya Elimu ngazi ya Halmashauri pamoja na Waratibu Elimu Kata Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya kwenye uzinduzi wa kukabidhi Mkakati wa Kuimarisha Ujifunzaji na Ufundishaji katika ngazi ya Elimu Msingi tarehe 09.09.2022 wilayani Chamwino.
Amesema kuwa shule za sekondari nazo zinatakiwa kuongeza ufaulu wa daraja la 1hadi 3 na kupunguza au kuondoa kabisa ufaulu wa daraja la 4 na daraja sifuri.
"Viongozi wa Elimu wasimamie nidhamu kwa wanafunzi na watumishi katika kuimarisha zoezi la ujifunzaji na ufundishaji katika taaisis zote aidha ushauri nasaha utolewe kwa wanafunzi ili waweze kukabiliana na changamoto watakazo kutana nazo katika ujifunzaji "amesema hayo Bi.Nyarege
Aidha Bi.Nyarege amesema kuwa wanafunzi watoro watambuliwe na warudishwe shuleni kupitia watendaji wa vijiji na Taarifa zitumwe katika ofisi ya Mkurugenzi kila ijumaa kabla au ifikapo saa 4 asubuhi ili ziweze kutumwa mkoani na wiki ya pili au inayofuata taarifa za idadi ya wanafunzi watoro waliorudi shuleni ziwasilishwe.
Bi Nyarege amesema "Ninafahamu kuwa Mwongozo ulizinduliwa rasmi tarehe 04.08.2022 mkoani Tabora na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye pia alizungumzia Malengo ya Mwongozo wa uandikishaji wanafunzi darasa la kwanza ili kuhakikisha wanafunzi walioandikishwa wanamaliza elimu ya msingi kama walivyoanza.
Pia amesema kuwa Viongozi katika ngazi zote wahakikishe walimu wanatambuliwa, wanathaminiwa na kuwezeshwa pamoja na kushirikishwa, kutiwa moyo na kutobaguliwa.
Mbali na hayo amewataka walimu kuonyesha ushirikiano na kujitathmini huku akitaka Uteuzi wa Viongozi wa Elimu kuzingatia Weledi, Uzoefu na Ubunifu katika ngazi zote.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.