Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imeweka mipango madhubuti na wezeshi ili kutokomeza suala la lishe duni kwa kuendeleza michakato mbalimbali ya kilimo cha mahindi katika shule za msingi na sekondari pamoja na kuendeleza bustani za mboga mboga shuleni ili kuondoa janga la utapia mlo.
Taarifa hiyo imetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Chamwino Bi. Neema Nyalege wakati akiwasilisha taarifa ya Halmshauri mara baada ya Mwenge wa Uhuru kumaliza ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokaguliwa katika wilaya hiyo.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya hadhara ya wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria kwenye mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Chamwino mwaka 2023 Bi. Nyalege amesema kuwa katika mwaka 2022/2023 hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano ni kuwa udumavu ni asilimia 0.2.
"Kwa kuzingatia mwongozo wa Taifa wa lishe kwa mwaka 2022/2023 hali ya lishe kwa watoto ni kama ifuatavyo udumavu ni 0.2 ukondefu ni 0.3 na uzito pungufu ni 0.7 na takwimu hizi zinaashiria kwamba utapiamlo unapungua kwa kasi katika Halmshauri ya wilaya ya Chamwino.
Bi. Nyalege ameongeza kuwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi millioni 96,566,000 kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe katika ngazi zote ikijumuisha Halmshaur,i Kata na Vijiji.
Aidha amezungumzia suala la mapambano dhidi ya rushwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kupitia njia za hadhara ikiwemo pia kupitia club za shule lengo ikiwa ni kuziba mianya ya rushwa .
Amesema kuwa kwa mwaka 2022/ 2023 TAKUKURU ilipokea malalamiko 76 na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ambapo mashauri 11 yaliendeshwa katika mahakama ya Chamwino na mashauri 7 kati ya hayo yametolewa hukumu.
Kuhusu suala la madawa ya kulenya amesema kuwa jeshi la polisi wilayani Chamwino kwa kufanya misako ya madawa ya kulevya jeshi hilo kuanzia mwaka July 2022 hadi July 2023 lilifanikiwa kukamata bangi kilo 24.0 kete 234 na misokoto 66 ambapo hadi sasa kesi 5 zimefunguliwa kituoni na watuhumiwa 12 wamefikishwa mahakamani na watuhumiwa wengine 13 bado upelelezi unaendelea.
Sanajri na hayo pia ameeleza hali ya ugonjwa wa maralia katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kubainisha kuwa kati ya mwaka 2020 hadi 2022 jumla ya wagonjwa 261,345 walipimwa vimelea vya maralia, kati ya hao watu elfu 24,934 sawa na 6.4% walikutwa na maralia ambapo wote walipatiwa matibabu na kutumia dawa kwa kipindi cha mwaka 2023 mpaka kufikia mwezi Septemba wagonjwa waliopimwa Malaria 8228 na waliogundulika kuwa na vimelea vya maralia ni 302 sawa na asilimia 3.7%.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.