Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ameongoza kikao cha Kamati ya Afya ya msingi ya Wilaya leo Agosti 30 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Lengo la kikao hicho ni kutoa taarifa na elimu kwa wajumbe juu ya kuchukua tahadhari ya mlipuko ugonjwa wa Mpox(homa ya nyani) ambao tayari umesharipotiwa kwenye baadhi ya nchi za Afrika Mashariki.
Imeelezwa kuwa ugonjwa huu unatokana na kirusi ambacho kinapatikana kwenye wanyama kama nyani na jamii zake, swala wa porini na panya.
Akizungumza katika kikao hicho Daktari Sophia Michael Nchimbi ameeleza kuwa tayari hatua zimeshaanza kuchukuliwa na Halmashauri ikiwemo kutoa elimu kuhusu kujikinga na ugonjwa huo kwa makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo watoa huduma za afya, vituo vya kutolea huduma za afya, mashuleni kwa Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani.
Vilevile barua zimepelekwa kwa viongozi mbalimbali wa dini ambao wanahudumia jamii kubwa ili waweze kutoa taarifa kwa waamini wao.
Aidha Kamati baada ya kupokea taarifa imejadili na kuweka mikakati ya wilaya itakayowezesha kukabiliana na ugonjwa ikiwa ni pamoja na wajumbe wote wa kamati kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwenye maeneo yao wanayoishi na hususani kwenye mikusanyiko.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.