Kamati ya Maafa Wilaya ya Chamwino imefanya kikao leo Novemba 30, 2023 kwa lengo la kuchukua tahadhari ya kudhibiti majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania ( TMA) ya uwezekano wa uwepo wa mvua za juu ya Wastani ( ElNino). Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Katika kikao hicho Mtaalam kutoka TMA ndugu Joseph J. Mgumba aliakwa na aliweza kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu hali ya hewa ikiwemo suala la matarajio ya uwepo wa mvua za juu ya wastani kwa Wilaya ya Chamwino kuanzia mwezi Desemba 2023 hadi Februari 2024.
Vilevile mtaalam wa TMA aliweza kueleza kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kuokana na uwepo wa mvua nyingi kama vile magonjwa ya mlipuko, uharibifu wa miundombinu ya barabara na majengo, kukatizwa kwa usafiri wa anga, athari za uchumi na mazingira.
Kupitia kikao hicho kamati imeweza kujadili na kuweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza katika kipindi hicho cha mvua.
Moja yamkakati ni TARURA kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja husani kwenye maeneo muhimu ya mapato na sehemu za kutolea huduma za afya yaani zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Ilijadiliwa pia kuhusu wananchi kupewa elimu kuhusu kutibu maji na matumizi sahihi ya vyoo ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Suala jingine lililopewa kipaumbele ni kununua dawa za kutosha kwaajili ya tahadhari ya magonjwa ya mlipuko ili ukitokea ugonjwa matibabu yaweze kutolewa.
Kwamaeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi kama Ikowa, Ingunguli kuhakikisha dawa na chanjo za kutosha zinanunuliwa na kupekwa vituo husika.
Kwaajili ya madhara ya ajali yanayoweza kutokea kutokana na athari za mvua kubwa ni kuhakikisha kunakuwa na magari ya wagonjwa muda wote pamoja na timu za dharura zitakazoweza kufanya kazi. Ilielezwa timu za dharura zimewkwa kituo cha Afya Chamwino, Hospitali ya Uhuru, Mpwayungu, Haneti, Mlowa barabarani na kusambaza namba za kitengo cha dharura cha afya kilichopo mkoani ambacho kinafanya kazi masaa 24 kwa wananchi ili linapotokea jambo kufanya mawasiliano.
Kamati pia imejiwekea mkakati wa kuyatambua maeneo yenye viashiria vya kutokea maafa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na maafa nà namna ya kuchukua hatua pindi yanapotokea ikiwa ni pamoja na kuziamsha kamati za maafa za kata na kuwaeleza majukumu yao.
Pia kubainisha ya kuwahifadhi watu iwapo maafa yametokea na hivyo kupelekewa huduma kwenye eneo hilo.
Aidhà ilielezwa kuwa wadau watakaoweza kusaidia pindi majanga yanapotokea wanapaswa kubainishwa ili kuweka urahisi wa kujua nani asaidiè kipi pindi majanga yanapotokea.
Vilevile ilikubalika kuwa elimu itolewe kwa madereva wanaondesha vyombo vya moto vya usafiri ili wachukue tahadhari kwa kipindi hiki ili kuepusha maaafa kwani panapokuwa na mvua nyingi barabara zinakuwa na utelezi, ukungu na pengine kukatika kwa barabara pamoja na madaraja. Hivyo tahadhari inatolewa kwa waendesha vyombo vya usafiri chamwino ili kuepusha maafa ni heri kusitisha safari pindi wanapoona hali ya hewa siyo nzuri au madaraja yamejaa maji kwa kufanya hivyo watakuwa salama.
Mkakati mwingine uliowekwa ni pamoja na kuwashauri wananchi kupunguza matawi ya miti yaliyokarobu na nyomba zao ili miti hiyo isiangukie nyumba na kuzibomoa.
Kwa upande utekelezaji wa miradi ya maendeleo ilikubaliwa kuwa vifaavyote vinavyohitajika kwenye mradi vinunuliwe vyote mapema na kupelekwa site ili hata itakapotokea maafa yoyote miradi isikwame kutekelezwa.
Kwa upande wa kilimo Serikali chini yauongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani suala la uwepo wa mvua nyingi wanalichukulia kama fursa na ndio maana wamejenga bwawa kubwa pale Membe kwa ajili ya umwagiliaji litakalochukua maji yanayotoka sehemu mbalimbali yaliyokuwa yakileta maafa mbalimbali kwa wananchi. Na kuna mpango mwakani wa kufanya ukarabati wa kuondoa tope kwenye mabwawa ya Manchali na Buigiri ambayo pia yatasaidia kupunguza maji yaliyokuwa yakifanya uharibifu.
Kutokana na uwepo wa maji mengi pia hupelekea ugonjwa wa ' riftvalley' kwa mifugo hivyo wafugaji na wananchi kwa ujumla waelimishwe pindi wanapoona mifugo inatoa mimba hiyo ni dalili mojawapo ya ugonjwa huo., hivyo watoe taarifa mapema mifugo ichanjwe kwani chanjo ni za bure.
Vilevile wananchi waendelee kuhimizwa kutunza chakula walichonacho kwani wakati mwingine kunapokuwa na mvua huwezi kuvuka kwenda sehemu nyingine na jukumu la kutunza chakula ni jukumu la familia.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.