Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imefanikiwa kutoa mkulima bora kanda ya kati kwa mikoa ya Dodoma na Singida. Hayo yalibainishwa kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (nanenane) kanda ya kati yaliyofanyika viwanja vya nanenane Nzuguni mkoani Dodoma.
Mkulima huyo anayejulikana kwa majina ya Aliseni Cosmasi Damian kutoka kijiji cha Magungu aliweza kulima hekari mia moja za zao la alizeti na mtama. Mkulima huyu aliongoza kwa kupata jumla ya alama 95%
Alipoulizwa kitu kilichomsukuma kuwekeza katika suala la kilimo Bwana Aliseni alieleza kuwa alisikia kwenye vyombo vya habari kuwa kuna uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula nchini, na hivyo akaamua kutumia fursa hiyo.
" Nilisikia kupitia vyombo vya habari vikitangaza kuhusu uhaba mkubwa wa mafuta ya kula, ndipo nikaona ipo haja yakutumia fursa hiyo." Alisema.
Vilevile alieleza kuwa kuhusu suala la Mtaji alisikia kupitia vyombo vya habari kuwa Halmashauri ya Chamwino inatoa mikopo kwa wakulima ikishirikiana na benki ya CRDB, kwa wakulima waliojiunga na AMCO's hivyo na yeye alipeleka mahitaji yake na alifanikiwa kuwezeshwa.
Aidha Bwana Aliseni ameishukuru sana Halmashauri ya Wilaya ya Chàmwino pamoja na benki ya CRDB kwa uwezeshaji huo na aliwashauri wakulima wengine wanaposikia fursa kama hizi wasisite kuzitumia kwani ndio njia ya kujiletea maendeleo.
Bwana Aliseni amesema anatarajia kupata wastani wa magunia 12 kwa ekari na hivyo kuwa na uwezo wa kulipa mkopo wa CRDB na kubaki na mapato kwa ajili ya kujikimu na shughuli nyingine za maendeleo.
" Matarajio yangu ni kupata gunia 12 kwa kila hekari baada ya mavuno ambapo nitaweza kurejesha mkopo wa CRDB na nitabaki pia na fedha kwa ajili ya kujikimu pamoja na shughuli za maendeleo." Alisema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.