• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Chamwino Yapongezwa Kupata Hati Safi Kwa Hesabu Za Mwaka 2023/2024

Imewekwa: June 16th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Staki Senyamule ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa kupata hati inayoridhisha (hati safi) kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi mwaka 2023/2024.

Pongezi hizo zimewasilishwa na Mhe. Janeth Mayanja Mkuu wa wilaya ya Chamwino kupitia hotuba aliyoisoma akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri yawilaya ya Chamwino wa kupitia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 uliofanyika leo Juni 16, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

" Mhe. Mwenyekiti naomba nitumie fursa hii kwa idhini yako niipongeze Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa kupata hati safi za ukaguzi zinazoishia 31 Juni 2024 ambayo inaifanya Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kuendelea kupata hati safi tangu mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024. Kitendo hiki kimeipa heshima Halmashauri  na Mkoa kwa ujumla. Hongereni sana kwa kazi kubwa mlioendelea kuifanya. " Alisema Mkuu wa Mkoa.

"Ninaamini mafanikio haya yamekuwepo kutokana na ushirikiano uliokuwepo kati yenu ninyi Waheshimiwa Madiwani, wataalam wa Halmashauri, viongozi na wadau mbalimbali wa Halmashauri. Hivyo nawasihi endeleeni kudumisha ushirikiano huo ili kuiwezesha Halmashauri ya Chamwino kuendelea Kupata hati safi katika kaguzi zote kila mwaka kama ambavyo imekuwa ni utamaduni. Alisema Mkuu wa Mkoa.

Pamoja na pongezi hizo ametoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha hoja zote ambazo hazijafungwa kuhakikisha zinajibiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria na maelekezo ya Serikali.

Mkuu wa mkoa pia ameipongeza Halmashauri kwa kukusanya mapato vizuri ambapo hadi kufikia Mei 31, 2025 ilikuwa imekusanya 96% ya mapato na kutoa rai kwa watendaji kuhakikisha wanakusanya mapato kwa asilimia zilizobaki na kuhakikisha miradi inasimamiwa na kukamilika.

" kwa taarifa ya uchambuzi wa ukusanyaji wa mapato iliyofanywa na mkoa taarifa  inaonesha kufikia 31Mei, 2025 Halmashauri ya Chamwino imekusanya mapato 96%, hivyo niwapongeze kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji. Niendelee kusisitiza kuongeza nguvu ya ukusanyaji naamini kwa muda uliobaki kuna mapato bado hayajakusanywa pamoja na kuongeza kasi ya kusimamia na kukamilisha miradi kwa wiki mbili zilizobaki kufikia Juni 30." Alisema Mkuu wa Mkoa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Tito P. Mganwa ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa, Wahe. Madiwani na Mkaguzi Mkuu wa nje wa hesabu za Serikali yaani 'Chief External Auditor'(CEA).

Nao viongozi wa Chama cha Mapinduziwakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mhe. George Malima na mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Dodoma Ndugu Yohana Musa wamepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Wahe. Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri. Aidha wamewaelekeza Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara kuhakikisha wanasimamia vema na kwa weledi shughuli zote za Halmashauri kwa kipindi ambacho Madiwani hawatakuwepo.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Yapongezwa Kupata Hati Safi Kwa Hesabu Za Mwaka 2023/2024

    June 16, 2025
  • Mheshimiwa Mayanja Aongoza Zoezi La kuteketeza Ekari Mbili Za Bangi Membe

    June 15, 2025
  • Chamwino Yaweka Mikakati Kuhakikisha Wanafunzi Wanamaliza Mzunguko Wa Elimu

    May 28, 2025
  • Wamiliki Mashine Za Kusaga Nafaka Wahimizwa Kufunga Vinyunyizi Vya Virutubisho

    May 26, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.