Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ambaye amekuwa mgeni rasmi katika kikao kazi cha kutambulisha Mradi wa EPIC katika wilaya ya Chamwino leo Oktoba 30, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri amesema wilaya imekubali na ipo tayari mradi huu utekelezwe ndani wilaya.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mhe. Mayanja amesema yeye binafsi na viongozi wenzake wa wilaya ya chamwino wanashukuru kwa kupelekewa mradi huu kwani kwa sasa Mashirika mengi yaliyokuwa yakifanya kazi za mapambano dhidi ya kupunguza maambukizi ya Virus vya UKIMWI yamepungua ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Ametoa shukrani na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.
"Tunawaahidi tutawapa ushirikiano wa kutosha ili malengo yenu yaweze kutimia. Tutawapa ushirikiano wa kutosha kwa sababu tatizo la UKIMWI lipo kwenye jamii yetu, na hasa nimefurahi kuona kwamba tajikita kuanzia kwenye makundi ya vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24. Ukiangalia takwimu zinaonyesha kundi hili ndilo kundi ambalo ni wahanga katika maabukizi kulingana na umri wao." Alisema Mhe. Mayanja.
"Lakini pia wapo katika kipindi cha ukuaji, kwa hiyo wamekuwa wakipitia changamoto nyingi. Wamekuwa katika kundi la hatari zaidi kupata virus vya UKIMWI kwa kuwa wapo kwenye ukuaji, hawajakomaa na wanashindwa kuhimili kupambana na changamoto wanazokutana nazo." Alisema Mhe. Mayanja.
Amewaomba pia kufanya tathimini watakapoanza kutekeleza mradi ili wautekeleze kulingana na changamoto za wilaya yetu kwani mazingira yanatofautiana kulingana na maeneo ya utekelezaji wa mradi.
Naye Meneja wa mradi mkoa wa Dodoma Ndg: Gideon Muganda ameleza namna mradi utakavyotekelezwa na lengo la mradi ambalo ni kudhibiti maambukizi ya Virus vya UKIMWI kwa makundi hatarishi ya rika balehe kuanzia miaka 15 hadi 24. Lakini vilevile alieleza inagusa pia kwa wanawake na wanaume walio kwenye mazingira hatarishi ya kupata Virus vya UKIMWI katika mazingira hatarishi kama vile maeneo ya migodi, uvuvi, shughuli za ujenzi, ilimradi tuyanawaweka katika mazingira ambayo ni rahisi kupata maambukizi ya VVU.
Lengo ifikapo 2030 watu wote wenye maambukizi 95%?wafahamu hali zao na wakishafahamu matarajio ni waweze kuunganishwa kwenye huduma ya matibabu na matunzo. Baada ya kuunganishwa kwenye matibabu inatarajiwa 95% ya Virus iwe imefubazwa kiasi kwamba wawe hawawezi tena kuambukiza na hiyo ndio faida ya kuwa kwenye dawa kwa muda mrefu. Ilielezwa kuwa kwa wale wasionamaambukizi ni tamanio wabaki hivyohivyo bila maambukizi kwa muda mrefu au kwa maisha yote.
Aliendelea kueleza kuwa wanafanya kazi kwa kutoa elimu ikiwemo elimu ya mabadiliko ya tabia, lakini pia kwa kuangalia uhatalishi watu walionao kulingana na mazingira wanayoyaishi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.