Wilaya ya Chamwino kupitia kikao chake na wadau mbalimbali wa elimu wamekuja na kampeni ya nishike mkono Chamwino kwa lengo la kukusanya zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 10 na vyumba 50 vya madarasa wilayani Chamwino.
Katika kikao hicho kilichosimamiwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Gift Isaya Msuya kimejumuisha wadau mbalimbali toka nje na ndani ya Wilaya ya Chamwino wamejadili mustakabali wa elimu katika wilaya ya Chamwino kwa kuweka mikakati mbalimbali itakayowezesha kupandisha kiwango cha elimu kwa shule za msingi na sekondari zilizopo Wilayani humo.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya amebainisha maeneo ambayo yatapewa kipaumbele katika awamu hii ya kwanza ya kampeni ya nishike mkono Chamwino ambapo watajenga mabweni 10 ili kuwasaidia wanafunzi hususani watoto wa kike wanaotumia umbali mrefu kufika shuleni.
Vilevile katika kampeni hiyo itawezesha ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa vipatavyo 50 ilikukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliopo hususani katika shule za msingi Wilayani hapo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wadau mbalimbali wamepongeza wazo alilokuja nalo Mkuu wa Wilaya wa kuona mbali suala la elimu katika Wilaya ya Chamwino na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha ilikutekeleza wazo hilo kwa vitendo ambapo zaidi ya Milioni moja ilichangwa papo hapo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.