Tathimini ya hali ya lishe ya Wilaya ya Chamwino kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka na kwa mwaka mzima imeonesha kufanya vizuri kwa vigezo vyote vya viashiria vya lishe.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 2, 2024 kwenye kikao cha tathimini ya lishe kilixhofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Licha ya kufanya vizuri mwenyekiti wa kikao mhe. Janeth Mayanja ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino amewasisitiza wajumbe wote kuhakikisha wanaendelea kuweka juhudi zaidi ili kuendelea kuwa kwenye nafasi nzuri.
Aidha wajumbe pia wamejadili na kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo suala la kutoa chakula shuleni kwa wanafunzi wote pamoja na kuendelea kuhimiza shule kulima bustani za mbogamboga na matunda.
Vilevile watendaji wa kata wametakiwa kushirikiana na maafisa ugani waliopo kwenye kata zao kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kulima kwa tija kwa kulima mazao yanayostawi kwenye kanda zao pamoja na kutumia mbegu bora.
Katika kikao hicho kata zilizofanya vizuri kwenye masuala ya lishe zilipewa zawadi ya vyeti na fedha kama motisha .
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.