Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wilaya ya Chamwino imefanya shughuli za usafi katika maeneo mbalimbali ya kata na vijiji leo jumamosi ya Aprili 20, 2024.
Kwa ngazi ya Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ndiye alieongoza zoezi hilo akishirikiana na kamati ya ulinzi na usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndugu Tito P. Mganwa, wakuu wa idara na wakuu waTaasisi pamoja na watumishi na wananchi wa Kata ya Chamwino.
Maeneo yaliyofanyiwa usafi ni kituo cha Afya cha Chamwino, stendi na sokoni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na viongozi wengine wa chama Tawala na Serikali wamewataka wananchi kudumisha tabia ya usafi kwenye maeneo wanayofanyia kazi na majumbani kwao kwani kwa kufanya hivyo wajiweka kwenye hali ya usalama na kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Zoezi hilo liliambatana na ugawaji miti kwa wananchi waliofika kufanya usafi ambapo TFS wamegawa jumla ya miche mia tatu ya miti.
Aidha Mkuu wa wilaya ametoa rai kuwa kwa wananchi watakaokuwa bado na uhitaji wa miche ya miti wasisite kuwaona TFS kwa ajili ya kupatiwa miche hiyo.
Vilevile amewashukuru wananchi kwa ushiriki wao nakuwaomba waendelee kuungamkono Muungano wetu na kuuombea uzidi kudumu kwani kuna nchi nyingi duniani ziliqnzisha muungano lakini hazikudumu. Aliwataka wajenge tabia ya kupenda vitu vya kwao kwanza.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Muungano ni MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI: "TUMESHIKAMANA NA TUMEIMARIKA KWA MAEND3LEO YA TAIFA LETU"
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.