Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imefanya mkutano wa mwaka na mashirika yasiyo ya Kiiserikali yanayofanya kazi wilaya ya Chamwino mapema wiki hii kwenye ukumbi wa Serikali ya kijiji uliyopo Chamwino.
Mgeni rasmi wa kikao hicho alikuwa Afisa Tarafa wa Tarafa ya Chilonwa ndugu Mohamed Mfaki ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya.
Katika hotuba yake mgeni rasimi aliwapongeza washiriki wote kwa kuitikia wito wa kushiriki mkutano huo wa mwaka wenye kauli mbiu "Uendelevu wa mashirika yasiyokuwa ya Kiserkali: Wadau tuwajibike."
Alieleza pia Serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza majukumu mbalimbali kuhakikisha changamoto katika jamii zinatatuliwa kwa wakati. Hivyo kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali itaharakisha kufikiwa kwa matokeo tarajiwa.
Vilevile alieleza kuwa mamlaka za Serikali za mitaa zinawajibu wa kusimamia mashirika yanayofanya kazi katika maeneo yao. Lengo la mkutano huo ni kukutanisha mashirika yote yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi katika wilaya ya Chamwino kwa pamoja ili waweze kujadiliana masuala mbalimbali katika kuboresha huduma kwa jamii na kuendelea kushirikiana kutekeleza miradi na programu mbalimbali hasa katika ustawi wa wanancni.
Alieleza kuwa Serikali inaendelea kusisitiza nia yake ya kuendelea kujenga na kuboresha mazingira wezeshi kwa masirika yasiyo ya Kiserikali nchini kufanya kazi kwa ufanisi na kuchochea maendeleo ya wananchi katika maeneo ambapo afua za mashirika zinatekelezwa.
Pia alisema Serikali inatambua wazi mchango na kazi kubwa wanayoifanya katika kuisaidia Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha alieleza kuwa mkutano huo ni fursa muhimu kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kujengeana uwezo kuhusu sheria na kanuni zinazoongoza mashirika yasiyo ya Kiserikali na Serkali pia kufahamu changamoto na shughuli zinazofanywa na mashirika ili kuwa na uelewa wa pamoja
Alitoa wito kwa mashirika kuendelea kuimarika kwa kufanya kazi kwa ufanisi na uzalendo, kufuata sheria na kanuni zake kwa manufaa ya maendeleo ya wilaya ya Chamwino. Serikali ipo tayari kupokea maoni na changamoto kupitia baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya Kiserikali yaani NaCONGO na wilaya ya Chamwino inao wajumbe watatu ambao waliwachagua.
Alisisitiza suala la kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji kwenye mipango yaoya kila mwaka hususani kuanzia kwenye kata na vijiji wanakotekeleza miradi. Alieleza pia si jambo jema kwa ofisi yake kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya sheriakutoka pande zote za Serikali na mashirika. Alishauri kila mmoja atumie kwa usahihi mifumo ya kiuratibu iliyowekwa kisheria na kanuni zake.
Alishaurikila shirika kuwa na mpango mkakati wa kupata fedha za kutekeleza shughuli zake kwa jutumia rasilimali za ndani zilizopo kuliko kutegemea wafadhili kutoka nje ya nchi. Hiyo itasaidia mashirika madogo kutofutiwa usajili kwa kushindwa kutekeleza miradi, kutoa taarifa za utekelezaji na kutolipa ada ya mwaka.
Aidha alieleza kuwa kumekuwa natabia ya mashirika yasiyo ya Kiserikali mengi kujikita maeneo ya mijini ambayo mara nyingi hayana changamoto kubwa kama ilivyo kwa maeneo ya vijijini. Alitoa wito kuwa ni vizuri washirikishwe wataalamu ngazi ya wilaya ili washauri wapi kuna uhitaji wa miradi.
Alisisitiza mashirika hayo kushirikiana na wataalamu wa Serikali ngazi zote kiwilaya ili kuhakikisha kunaiuwa hakuna mwingiliano wa na migongano ya kiutendaji na kiuratibu katika kufikia azima ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa uharaka.
Katika mjutano huo mambo mbalimbali yaliweza kujadiliwa ikiwemo utendaji kazi wa mashirika hayo, mafanikio na changamoto wanazopitia.
Pia wajumbe walijadili na kuweka mikakati itakayoboresha utendaji kazi wao hususani katika suala la utoaji wa taarifa za utendaji wao wa kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.