Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo tarehe 30 Oktoba 2024 imeadhimisha kilele cha siku ya lishe kitaifa katika kata ya Ikowa kijiji cha Makoja.
Maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa kitaifa nchi nzima na katika Wilaya ya Chamwino yalilenga kutoa elimu juu ya lishe bora kwa jamii hasa lishe bora kwa watoto.
Akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo diwani wa kata ya Ikowa Mh. Emmanuel Anderson, amewahasa wananchi wa kata ya Ikowa kuzingatia afya kwa kuwasisitizia kuwa afya bora ndio mali namba moja kwa binadamu na hivyo kuwataka kuzingatia vyakula ambavyo vinaelekezwa na wataalam kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Sanjari na hilo, Mh. Emmanuel Anderson amewataka wananchi hasa wanaume kuondokana na dhana potofu ya kuamini kuwa masuala ya lishe ni masuala yanayohusu wanawake pekee, hivyo amewaomba wanaume kujitokeza na kushiriki katika masuala ya lishe kwani kufanya hivyo kutawawezesha kutambua faida ya lishe kwa mtoto, mama na kwao wenyewe.
Kwa upande wa Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Rachel Magafu amewaomba wazazi kujitokeza na kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata chakula muda wa shule kwani kutawafanya wanafunzi kusoma katika hali nzuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.