Baraza la Madiwani kupitia mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la kujadili Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025-2026 kwa pamoja limepitisha bajeti ya jumla shilingi bilioni 50,617,686,000 ya Halmashauri leo tarehe 27 Februari, 2025.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri umepitisha bajeti hiyo ya bilioni 50.6 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 5.00 ikilinganishwa na mwaka 2024-2025.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri Bw. Geofrey MacKenzie kwa upande wa mapato ya ndani Halmashauri inakisia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 4.3 ambayo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 2.5 ni mapato halisi na shilingi bilioni 1.7 ni mapato lindwa.
Aidha, katika makisio ya makusanyo ya mapato ya ndani halisi ya Halmashauri ya shilingi bilioni 2.5, kiasi cha shilingi bilioni 1.03 sawa na asilimia 40 kitaelekezwa katika miradi ya maendeleo na kiasi cha shilingi bilioni 3.2 kitaelekezwa kwenye matumizi ya kawaida ikiwa ni uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na gharama za uendeshaji wa Halmashauri.
Kufuatia kuwasilishwa kwa bajeti hiyo, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Edson Sweti wamepongeza bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2025-2026 kwa kugusa maeneo muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya Wananchi na Halmashauri kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.