Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imefanya mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya kwanza Novemba 15-16, 2023. Mkutano umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Edson M. Sweti.
Katika mkutano huo mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo suala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri pamoja na utekelezaji wa miradi na program mbalimbali za maendeleo.
Ilielezwa kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri kupitia program mbalimbali ilidhinishiwa kiasi cha shilingi 14,519,291,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi na program mbalimbali za maendeleo. Hadi kufikia Septemba 2023 Halmashauri imepokea julma ya shilingi 2,652,338,725.00 sawa na asilimia 18 ya bajeti iliyoidhinishwa.
Aidha Wahe. Madiwani waliwaelekeza taasis ya TANESCO kutenga siku maaalum ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli zao kwa Wahe. Madiwani ili waweze kama zinavyofanya Taasis nyingine kama vile RUWASA.
Ilielezwa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kuwa na uelewa wa pamoja ikiwa ni pamoja na kuwaeleza wananchi utekelezaji uliofikiwa na hivyo kuwa na majibu pindi watapohojiwa na wananchi.
Naye mwakilishi wa Meneja wa TANESCO Wilaya alikubaliana na hoja hiyo ya Wahe. Madiwani na kuahidi kutekeleza kuanzia rbo inayofuata.
Kwenye kikao hicho pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya alitumia aliwakumbusha Madiwani kuzungumzia mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita hususani kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kata zao kupitia mikutano ya hadhara.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.