Tarehe 23 Desemba 2019, Baraza la Biashara limefanya kikao kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ikiwa na lengo la kukutanisha sekta ya umma na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya biashara.
Wajumbe wa baraza hilo wametoa wito kwa wafanyabiashara wa nje na ndani ya Chamwino kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Wilayani hapa na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kufanya uwekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti Mwenza wa Baraza Bwana Richard Mmasi amesema kuwa zipo fursa za nyingi uwekezaji ikiwa ni pamoja na kilimo cha zabibu na mazao mengine, mifugo na madini.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Juliana Kilasara ameeleza kuwa ni wakati sahihi kwa baraza kujipanga kutoa elimu kwa wanyabiashara ngazi ya Vijiji na Kata ili kuwapa fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili ili serikali iendelee kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiasha.
Nae Meneja wa TRA Wilaya ya Chamwino Ndugu Omari Rajabu ametoa wito kwa wafanyabiasha na wananchi wanaostahili kulipa kodi ya majengo ambayo ni shilingi 10,000 kila mwaka.
Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa baraza la biashara ni kuwakutanisha viongozi wakuu wa Wilaya kutoka Sekta Binafsi na Serikali chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwaajili ya kukuza uchumi kutumia sekta binafsi. Hususan katika ngazi ya Mikoa na Wilaya,
Malengo mengine ni Kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara na uwekezaji, Kuibua Fursa za uwekezaji na Kuzinadi fursa hizo – kupitia Kongamano za Uwekezaji nakadhalika.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.