Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja leo terehe 30 January, 2025 amewahimiza Waheshimiwa Madiwani kufuatilia wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ambao hawajaripoti katika shule walizopangiwa ili kuanza masomo.
Mhe. Janeth Mayanja ametoa wito huo kupitia mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambao ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Niwaombe sana Waheshimiwa Madiwani kupitia mkutano huu kazi ya ufuatiliaji kabla ngazi ya Wilaya hatujaanza kufanya ufuatiliaji nyinyi ni wenyeviti wa kamati za maendeleo ya kata, wanafunzi kwenda kuripoti wale wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza hayo nayo ni maendeleo”. Amesema Mh. Mayanja.
Sambamba na hilo, Mh. Mayanja amesema baada ya tarehe 10 Februari, 2025 ofisi ya Mkuu wa Wilaya itaanza kuchukulia hatua wazazi na walezi wenye watoto ambao walitakiwa kuripoti shule na wao kuwapa majukumu mengine.
“Baada ya tarehe 10 tutachukua hatua kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi wenye watoto ambao walitakiwa wawepo shule lakini wao wamewapa majukumu mengine, lakini sasa tufanye utawala bora kwa kupita nyumba kwa nyumba”. Amesema Mh. Mayanja.
Aidha, katika kukabiliana na hali ya uhaba wa mvua Mkuu wa Wilaya amewataka Waheshimiwa Madiwani kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kupanda mazao yanayostahimili mvua chache ikiwemo zao la alizeti pamoja na mtama katika muda uliobakia.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.