Wawakilishi wa shirika la msaada la Uingereza UKAID(FCDO) ambalo linafadhili mradi wa Shule Bora na EP4R limefanya ziara Wilayani Chamwino leo Desemba 1, 2022 kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa mradi wa Shule Bora na kupata maoni ya watendaji wa Serikali kuhusu jinsi ya kutekeleza mradi kwa ufanisi zaidi.
Katika ziara yao wametembelea makao Makuu ya Ofisi ya Halmashauri iliyopo Buigiri pamoja na shule kwa lengo la kukagua mafanikio wa mradi uliopita wa EQUIP - T.
Vilevile wamepanda miti ya mwembe kwenye eneo la Ofisi ya Halmashauri na shule ya msingi Mblenzungu kama ishara ya urafiki na ushirikiano wa dhati kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza.
Shule zilizotembelewa na wageni hao ni pamoja na shule ya msingi Mbelenzungu, Mnase na Msamalo.
Mradi wa Shule Bora unalenga kuiunga mkono Serikali ya Muungano wa Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wote wa kike na wakiume katika shule za Serikali za Tanzania.
Kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania mradi huu utafanya maboresho yatakayowezesha kila mtoto kupata msingi mzuri katika elimu yakeya awali ili kuitumia fursa kwa kutoa mchangowake katika ukuaji wa nchi na maendeleo yake.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.