Timu ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Umma wamefanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino ikiwa na lengo la kujifunza jinsi Halmashauri inavyotekeleza majukumu yake hususani kwenye ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo na katika kujifunza huko wataweza kuboresha utendaji kazi wa kazi za Serikali. Ziara hii imefanyika Novemba 24, 2022.
Kabla ya kwenda kutembelea maeneo husika walifanya kikao na menejimenti ya Halmashauri na ujumbe huo ukiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Jaji Amisa Kalombora walielekeza watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kwani tume isingependa kuona watumishi wanafukuzwa kazi kwani ni hasara kwa Serikali na kwa watumishi wenyewe.
Aidha aliwaelekeza watumishi kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza mapato na iwapo kunakuwa na changamoto zitatuliwe kwa wakati kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Vilevile alieleza kuwa wamebaini watumishi kufukuzwa kazi kutokana na kifaa cha kielektroniki cha kukusanya mapato(POS) na kutokana na hilo tume imeamua kufanya ziara ili kujifunza kutoka kwa wadau wenyewe.
Waajiri pia waliaswa kuzingatia sheria, kulinda na kuzingatia haki za watumishi na kwa kufanya hivyo hakutakuwa na malalamiko ya watumishi.
Mwenyekiti pia alieleza kuwa wanajua kuna mamlaka za nidhamu ambazo hazitekelezi majukumu yao na kupelekea mashauri ya nidhamu kuanza upya kutokana na kutozingatia taratibu za mashauri ya kinidhamu na kusababisha hasara kwaSerikali. Aoieleza kuwa Tume inawakumbusha majukumu yao na piawanakumbushwa kuwasilisha vielelezo vya mashauri kwa wakati.
Kwa mamlaka ambazo hazijatekelezamaagizo ya tume zimeagizwa kutekeleza maaagizo hayo ndani ya siku 14 kuanzia Novemba 24, 2022.
Pia Mwenyekiti alieleza kuwa tume imebaini bado kuna mapungufu katika kutekeleza na kushughulikia masuala ya utumishi wa Umma kwa baadhi ya waajiri yanayopelekea watumishi kushindwa kujua majukumu yao na kuwakosesha haki watumishi hususani kwa waajiriwa wapya na kupelekea malalamiko yasiyo ya lazima.
Aliwaasa watumishi kuzingatia viapo vyao likiwemo sualala kutunza siri za Serikali na wanaovunja viapo vyao wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Watumishi walitakiwa kutofanya kazi kwa mazoea na kwa manung'uniko. Kunapokuwa na mapungufu wawaendee viongozi wao na kuwaeleza mapungufu hayo ili yashughulikiwe.
Katika ukaguzi uliofanyika wa POS na ujenzi wa madarasa wajumbe walilidhishwa na utekelezaji na kuipongeza Halmashauri kwa kazi nzuri na kuwaomba waendelee na ari hiyohiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.