Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amehaidi kupeleka umeme katika vitongoji vyote katika Wilaya ya Chamwino.
Mhe. Dkt. Biteko ametoa ahadi hiyo leo tarehe 2 Februari, 2025 alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa CCM jimbo la Chamwino wakati Mbunge wa jimbo la Chamwino na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. Deo John Ndejembi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana Manchali.
“Mnavyo Vitongoji 355 katika Wilaya yenu tupeni muda tunafanyia kazi tumemaliza kupeleka umeme katika vijiji vyote mlivyonavyo tunahamia kwenye vitongoji, tumeanza na vitongoji 15 baadae tutakuja vitongoji vingine vyote tutavipelekea umeme”. Amesema Mhe. Dkt. Biteko.
Akiendelea kuzungumzia sekta ya Nishati nchini Naibu Waziri Mkuu amesema mwaka 2024 Tanzania iliongoza katika upelekaji wa nishati ya umeme kwa wananchi.
“Niwape habari njema mwaka jana Benki ya Dunia ilitupima Tanzania katika upelekaji wa nishati ya umeme kwa Wananchi Tanzania tuliongoza na ndio maana mmeona mkutano mkuu wa wakuu wa nchi barani Afrika umefanyika Tanzania sio kwa bahati mbaya kwasababu tunatafuta pesa kwaajili ya kupeleka nishati ya umeme kwa watu”. Aliongeza Mhe. Dkt. Biteko.
Aidha, katika mkutano huo pia Mhe. Dkt. Biteko amehaidi kulifanyia kazi suala la ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya ya Chamwino.
“Nataka nikuhakikishie Mhe. Deo Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mipango yake kwenye sekta ya afya kujenga hospitali za Wilaya na lenyewe tutalichukulia kwa uzito wake nataka niwahakikishie litafanyiwa kazi.”
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.