Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki zoezi la kuboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la wapiga kura leo Mei 17, 2025 katika ofisi ya Kijiji cha Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mhe. Rais ameshiriki zoezi hilo la kuboresha taarifa ili aweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 katika kituo hicho kwa kuwa yeye ni mkazi wa Wilaya ya Chamwino.
Aidha, amewahasa Wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata haki yao ya kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Zoezi hilo limeanza jana Mei 16 na litatamatika Mei 22, 2025 ambapo vituo vyote vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.