Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Isaya Msuya ametoa rai kwa Wahe. Madiwani kuhakikisha wanachukua tahadhari dhidi ya mambo madogo madogo ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao. Ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Novemba 8, 2022. Alieleza kuwa iwapo atatokea mtu anataka kuharibu amani taarifa itolewe ili aweze kuchukuliwa hatua.
" Ni vema tukachukua tahadhari ya mambo madogo madogo ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yetu. Tukionamtu yeyote anataka kuharibu amani, tulitolee taarifa suala hilo ili achukuliwe hatua." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Alieleza pikuwa kuna baadhi ya viongozi wanaoongoza migomo na maandamano na kusema Serikali haiongozwi kwa mihemuko. Aliongeza kusema kuwa Serikali tayari imeanza kuchukua hatua kwa viongozi hao
Vilevile Mkuu wa Wilaya alisisitiza kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato kwani fedha zinahitajika kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo, na kueleza kuwa Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo kwa kila Halmashauri kuhakikisha inakusanya kwa 100%. Alieleza kuwa Madiwani wakiamua hawawezi kushindwa kukusanya kwa 100%.
" Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa hangependa Halmashauri ikusanye chini ya 100%." Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mkuu wa Wilaya alitilia mkazo kuhusu suala la kukamilisha miradi ya ujenzi wa madarasa kwa wakati kulingana na muda wa kukamilisha uliowekwa na mkoa wa tarehe 31, Novemba 2022.
Alisisitiza pia kuhusu suala la umoja na mshikamano kwani maendeleo wanayoyafanya ni kwa ajili ya manufaa ya wananchi. Aliomba kila mmoja afanye kazi kwenye mipaka yake na kuwe na kuheshimiana.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.