Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Chini ya Ufadhili wa serikali ya Norway kinatekeleza mpango wa Local Climate Adaptive Living Facility (LoCAL) wenye lengo la kujenga jamii zenye uhimilivu zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Kupitia mpango huu, LGTI imezindua mafunzo ya kujenga uwezo kwa kikosi kazi cha Halmashauri (Council Task Force (CTFs)) na Wawezeshaji wa Kata (Ward Facilitator (WFs)) kuhusu kujenga ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mbinu ya O&OD iliyoboreshwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Tito P. Mganwa tarehe 21 Julai 2025, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuisha masuala ya tabianchi katika kuibua, kupanga, kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii inayolengwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuwa na usalama wa chakula.
Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa sasa inatekeleza awamu ya pili ya LoCAL kupitia Mradi wa KILIMO HIMILIVU mpango wa mwaka mmoja (Julai 2025 – Juni 2026). Mradi huu unalenga kata za Msamalo na Mvumi Makulu, ukihimiza kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi, matumizi endelevu ya ardhi na usimamizi bora wa maji, ili kusaidia jamii za wakulima na wafugaji kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.