Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vija, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana kuzitumia fursa zinazotolewa na Serikali ili kujiletea maendeleo katika mazingira wanayoishi.
Akizungumza katika kongamo la vijana lilifonyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino 28, Oktoba 2022, amesema wajibu walio nao Ofisi ya Waziri Mkuu wanaojihusisha na ajira kwa vijana kuwa wanahakikisha wanabadilisha mtazamo kwa vijana.
Mhe. Katambi amesema Serikali ina wajibu wa kutimiza yale yanayotakiwa kwa vijana na wanapaswa kufanya mambo ambayo yatawaletea manufaa baadaye.
“Wajibu mkubwa tulionao Ofisi ya Waziri Mkuu wanaoshughulika na masuala ya vijana ni kuhakikisha tunabadilisha mitazamo na tuwe na mitazamo chanya kwa vijana na kubadilisha mitazamo, fikra sio jambo rahisi".
“Kwamba Serikali inatengeneza mazingira wezeshi ya kuwasaidia vijana na kuhakikisha wale vijana ambao wako kwenye masuala ya kujikwamua kiuchumi inaweka progamu mbalimbali pia kijana fanya mambo ambayo jamii itakuelewa baadaye na hatakama sio baadaye itaelewa kwa mambo mema unayofanya,” amesema.
Katambi amesema vijana wanapaswa kufuatilia na kujua utaratibu wa kujipatia mikopo kupitia fungu linalotengwa na Serikali kupitia Afisa maendeleo ya vijana na Afisa maendeleo ya Jamii ambao wapo kwenye maeneo yao ya Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi
Hata hivyo amesema vijana wanapaswa kujiunga na vikundi ili waweze kupata mikopo hiyo na kuzitumia kwa malengo endelevu katika jamii
Amesema pia Serikali imeweka mpango wa mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.
“Serikali imeanzisha sheria nyingine ya fedha za Halmashauri ambapo kutakuwa na mgawanyo wa asilimia kumi (10%) ya mapato ghafi ya Halmashauri, asilimia kumi (10%) kila mwaka zitengwe kwaajili ya shughuli za vijana, kwa vijana tunapata asilimia nne (4%), kwa wanawake asilimia nne (4%) na kwa watu wenye ulemavu asilimia mbili (2%) na sharti ni kwamba mjiunde katika makundi ya vijana kumi (10) ili mpewe fedha hizo na zimekuwa zikitoilewa nchini kote.
“Ni wewe tu kufuatilia fursa na kuweza kupata taarifa rasmi kupitia Afisa maendeleo ya vijana na Afisa maendeleo ya Jamii ambao wapo kwenye maeneo yetu, fedha zinatolewa lakini changamoto pia imekuepo hatuzi tumii vizuri au hatuhamasiki kwenda lakini pia vijana hatujitokezi kwenda kujiunga kwenye vikundi, sasa hapo ni kwa aliye soma na siyesoma Serikali imekuwekea mpango,” amesema.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.