Kamati ya Siasa Wilaya ya Chamwino ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. George Malima ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chamwino imekagua miradi ya maendeleo katika jimbo la Mvumi jana tarehe 12 Machi, 2025.
Kamati hiyo ambayo iliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mh. Janeth Mayanja pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri na taasisi zingine za Serikali Wilaya ya Chamwino imekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Igandu, ujenzi wa Shule ya Msingi Ilolo, ujenzi wa madaraja mawili ya mawe kata ya Muungano pamoja na mradi wa REA kijiji cha Idifu, kitongoji cha Muungano.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Ndg. George Malima amepongeza jitihada zinazofanywa za kuanzishwa na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kuwahasa Wananchi kuilinda miundombinu hiyo.
Aidha, Ndg. Malima amepongeza jitahada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.